Loading ...
Sorry, an error occurred while loading the content.

Mikakati ya Kuimarisha Hakielimu rafiki mwaka wa 2010

Expand Messages
 • Josephat Ndibalema
  Ndugu Marafiki,   Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2010, ni matarajio yangu kuwa mwaka wa jana yaani mwaka 2009 umemalizika salama.
  Message 1 of 1 , Jan 13, 2010
  • 0 Attachment
   Ndugu Marafiki,
    
   Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2010, ni matarajio yangu kuwa mwaka wa jana yaani mwaka 2009 umemalizika salama. Pia napenda kuwapa pongezi wale wote walioshiriki katika kuhabarisha kupitia Hakielimu rafiki http://groups.yahoo.com/group/HakiElimuRafiki  , mawazo yenu yana dhamani kubwa sana ni matarajio yangu kuwa waliosoma mawazo yenu wamefanikiwa kwa kuelimika kupitia mawazo hayo.
    
   Ni faraja kwangu pia kwamba Hakielimu rafiki sasa imefikisha miaka miwili na miezi sita toka nilipoanzisha kikundi hiki tarehe 27/7/2007, hata hivyo pamoja na kufanya kazi kwa muda wa miaka miwili na miezi sita bado idadi ya wanachama pamoja na ushiriki wao ni mdogo . Sasa kupitia ujumbe huu nawaasa wale wote waliojiunga na Hakielimu rafiki wajitaidi kushiriki kwa kuendeleza mijadala mbalimbali juu ya masuala yanayohusiana na maisha yetu ya kila siku. Changamoto ni nyingi katika maisha yetu ya kila siku; je tufanye nini ili tuweze kupunguza au kuondoa changamoto zinazotukabiri.
    
   Baadhi ya changamoto tulizo nazo kwa sasa ni elimu duni,mabadiliko ya tabia nchi/hali ya hewa; ongezeko la maradhi kama ukimwi,ugonjwa wa malaria, uduni wa huduma za jamii, muanguko wa maadili katika jamii yetu,ongezeko la umaskini hasa kwa watu waishio vijijini,uhaba wa maji,ubovu wa miundombinu,kilimo duni,,,je tufanye nini?; Lakini pamoja na hayo mimi nimekuwa nikisisitiza mara kwa mara kuwa swala la elimu kwa umma linatakiwa kupewa kipaumbele na serikali pamoja na jamii nzima. Hizi ni changamoto zilizoko mbele yetu,kwa sasa  dunia imekuwa kama kijiji kutokana na maendeleo ya teknolojia hasa teknolojia ya habari na mwasiliano, ni vyema kama tutatumia fursa hii kiungunganisha nchi yetu na atimaye dunia kwa kujifunza toka kwa wengine walioweza...Hata sisi tunaweza.
    
   Pamoja na hayo napenda kuwafahamisha kuwa ifikapo march mwaka 2010 jina la Hakielimu rafiki  litabadilika na kuwa "Haki ya Elimu Forum" na itatakiwa kila mwanachama kujiunga upya kwenye Haki ya Elimu Forum, nitajitahidi kueleza sababu za kubadilisha jina toka Hakielimu rafiki na kuwa Haki ya Elimu Forum,pia nitatoa tathmini ni kwa kiwango gani wanachama waliopo wameweza kushiriki baada ya hapo juhudi zitafanyika kutangaza na kupata wanachama wengi zaidi wenye nia ya kuinua kiwango cha elimu Tanzania. Tujifunze na tuwafundishe wengine kupitia Hakielimu rafiki
    
   Hakielimu rafiki working group manager
   Josephat Thobias Ndibalema


   Be smarter than spam. See how smart SpamGuard is at giving junk email the boot with the All-new Yahoo! Mail
  Your message has been successfully submitted and would be delivered to recipients shortly.