Skip to search.
uislamu

Group Information

  • Members: 64
  • Category: Islam
  • Founded: May 16, 2005
  • Language: English
? Already a member? Sign in to Yahoo!

Yahoo! Groups Tips

Did you know...
Message search is now enhanced, find messages faster. Take it for a spin.

Messages

  Messages Help
Advanced
Jifunze Uislamu kupitia mtandao, tarehe 29 Safar 1433   Message List  
Reply Message #170 of 173 |



Last Update :   23 Januari 2012 (Jumatatu)
    29 Safar (Mfungo Tano) 1433 AH

Makala
Uislamu-Utangulizi
Fiqhi na Sheria 
Akhlaaq-Tabia
Sira ya Mtume
Nasaha za dini
Maswali na Majibu  
Uliza Suala la dini
Jiunge  !!!
 
 
  Karibu kwenye Mtandao wa UISLAMU  

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui...." 96:1-5








Dondoo za wiki

Ulazimu wa Waqfu na hukumu zinazo uandamia 
Waq-fu ni miongoni mwa vifungu lazimishi ambavyo vinavyo andamiwa na athari zake (vifungo hivyo), mara tu kinapo anzishwa (fungwa) kifungo kilicho sahihi. Na waq-fu si kama wasiya, kwani huo (wasiya) ni kifungo juzishi.
Ulazimu wa kifungo cha waq-fu unaandamiwa na hukumu zifuatazo:
1. Kutokuthibiti kwa khiari katika kifungo cha waq-fu. Angalia, mtu atakapo funga waq-fu ulio sahihi katika sheria, hatakuwa na khiyari majlisi kama ambavyo pia asivyo kuwa na khiyari sharti..
Endelea ....


Haya (Soni) ...Inaendelea 
Hakika haya ni muhimili wa kheri na ni elementi katika kila tendo linalo ichafua, Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: "Uchafu haukuingia katika kitu ila hukitia towa na haikuwa haya katika kitu ila hukipamba kitu hicho". Tirmidhiy-Allah amrehemu.
Endelea .....


Sayyidna Uthman aasiwa
Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-alikuwa akiutahadharisha umma wake dhidi ya kuibua na kuchochea fitina miongoni mwake. Na ni mara nyingi tu alikuwa akitoa tahadhari dhidi ya fitina, kwa sababu nguvu ya umma pale itakapo gurishwa kutoka kwa adui na kuletwa kwa wana wa umma wenyewe, hali ya umma huo itakuwa ni mbaya na nidhamu/mpangilio wake utafisidika. Na umma huo utakuwa karibu mno na uhovyo hovyo/fujo/ghasia na mbali mno na utengefu/ukaa sawa/ushwari.   Endelea ...


Mazungumzo baina ya Mitume na kaumu yao ...Inaendelea
Na mahala pengine tunaiona aina nyingine ya mdahalo/majadiliano yaliyo jiri baina ya Mtume Shuaib-Amani imshukie-na kaumu yake. Na majadiliano haya yamekuja kwa sura yenye ufafanuzi zaidi kuliko yale yaliyo tangulia, hebu yasikilize kupitia kauli yake Allah Ataadhamiaye: "NA KWA WATU WA MADYANA TULIWATUMIA NDUGU YAO SHUA'IB AKASEMA: ENYI WATU WANGU! MUABUDUNI ALLAH. NYINYI HAMNA MUNGU ILA YEYE, WALA MSIPUNGUZE VIPIMO NA MIZANI. MIMI NAKUONENI MMO KATIKA HALI NJEMA, NAMI NAKUKHOFIENI ADHABU YA SIKU KUBWA HIYO ITAKAYO KUZUNGUKENI. NA ENYI WATU WANGU! TIMIZENI VIPIMO NA MIZANI KWA UADILIFU WALA MSIWAKHINI WATU VITU VYAO; WALA MSIENEZE UOVU KATIKA NCHI MKAFANYA UHARIBIFU. ALIVYO KUBAKISHIENI ALLAH NDIYO BORA KWA AJILI YENU, IKIWA NYINYI NI WAUMINI. WALA MIMI SIYE MLINZI WENU". [11:84-86]  Endelea ...


 

Nyakati za Swala
Tafsiri ya Qur-an

Aya ya Wiki

"JE! HAWAKUONA KWAMBA TUNAIFIKIA ARDHI TUKIIPUNGUZA NCHANI MWAKE? NA ALLAH UHUKUMU, NA HAPANA WA KUPINGA HUKUMU YAKE, NAYE NI MWEPESI WA KUHISABU". [13:41]

 


Hadith ya Wiki

Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie-amesema: "Lau mwanaadamu angeli kuwa na mali iliyo jaa majangwa mawili, basi angeli taka na la tatu. Na wala tumbo la mwanaadamu halitajazwa ila na mchanga na Allah huipokea toba ya mwenye kutubia". Bukhaariy & Muslim-Allah awarehemu.

 


Katazo la Wiki

Ewe mwanamke wa Kiislamu, kwa nini humuogopi Mola Mlezi wako?! Mume hukuchaguliwa na mtu, umempenda mwenyewe, akaja kwa wazazi, ukaozeshwa. Kwa nini leo unampa mgongo kitandani?! Acha mara moja, kwani huko ni kuzinunua bure laana za malaika, viumbe wasio muasi Allah, sikia na utafakari: "Mume atakapo muita mkewe kitandani kwake, naye asimuitike, (mume) akalala akiwa amemghadhibikia. Hulaaniwa (mwamamke huyo) na malaika mpaka kunapambazuka". Bukhaariy & Muslim-Allah awarehemu.

 

Swali la Wiki

SWALI: Nini hukumu ya udhu kwa mwanamke aliye zitia kucha zake hiki kinacho itwa leo "rangi ya kucha"?

 

JIBU: Hakujuzu kwa mwanamke anaye swali kupaka rangi kucha zake ikiwa rangi hiyo inayazuia maji kukufikia kiungo wakati wa kuchukua twahara ya udhu au josho. Na kila kitu kinacho zuia maji kufika kwenye kiungo kinacho twaharishwa, hakijuzu kutumiwa na mwenye kutawadha au mwenye kuoga, kwa sababu Allah Ataadhamiaye anasema: "...BASI OSHENI NYUSO ZENU, NA MIKONO YENU..." [05:06]

Na mwanamke akiwa amezipaka rangi kucha zake, bila ya shaka rangi hiyo inayazuia maji kukifikia kiungo kinacho oshwa, kwa ajili hiyo basi anakuwa bado hajauosha mkono wake. Na kwa kitendo chake hicho cha kutokukamilisha kuosha kiungo cha udhu, anakuwa ameiacha mojawapo ya nguzo za udhu/josho.

Allah ndiye Mjuzi mno.



| Tuandikie |



:

Mon Jan 23, 2012 12:42 pm

uislamu-owner@yahoogroups.com
Send Email Send Email

Message #170 of 173 |
Expand Messages Author Sort by Date

Last Update : 23 Januari 2012 (Jumatatu) 29 Safar (Mfungo Tano) 1433 AH Makala Uislamu-Utangulizi ...
uislamu-owner@yahoogr... Send Email Jan 23, 2012
12:42 pm
Advanced

Copyright © 2010 Yahoo! Inc. All rights reserved.
Privacy Policy - Terms of Service - Guidelines NEW - Help