Enyi wanazuoni weledi,
Amani iwe nanyi
Napenda kumpongeza jukwaani mwanazuoni Evaristo Haulle kwa 'kukataa kufa'.
Amekataa kufa kwa kutoenda kuuza mchicha ama kuanzisha dirisha la kuuza sabuni pale nyumbani kwake, aitwe mjasiriamali.
Amekataa kufa kwa kugomea kunyamaa afe kibudu;
Amekataa kufa kwa kukionea haya Kiswahili lugha adhimu ya Taifa;
Mwenzetu kakataa kufa, amechapisha Diwani yake ya kwanza; ULIZA TU (kitabu cha mashairi),
amekataa kufa, amekibinua kiulizo!
Onja Ladha ya yaliyomo:
MAHABA
Mahaba ni kama moto, joto utafurahia
Mahaba ni kama moto, chakula utapikia
Mahaba ni kama moto, mwanga tajipatia
Mahaba ni kama moto pia unaangamiza,
Mahaba ni kama maji, mwilio wahitajia
Mahaba ni kama maji, kiu yatakukatia
Mahaba ni kama majiukikosa wajutia
Mahaba ni kama maji, yazoa yaangamiza
KAMA KWELI WAFAA:
Kama kweli unafaa, khanga vitenge vya nini?
Kama kweli unafaa,huhitaji bilioni
Kama kweli unafaa, huna haja kurubuni
Kama kweli unafaa, waonekana machoni.....
Na
WAFALME MWITUNI
Tembo na miguvu yako, ni vipi unatishika
Ndani ya himaya yako, kichwani unajishika
Tazama unyayo wako, sisimizi watishika
Ni nini uoga wako, waache waandamane.
Langu ni neno la pongezi kwako mwanazuoni Evaristo, changamoto umenipa.
Ninazo nakala chache kwa walioko Dar waweza kujipatia.
Adam

2 of 2 Photo(s)